Trick mbali mbali za simu
Wengi hukumbwa namatatizo katika simu zao ambayo kama yakiachwa basi huaribu mfumo
mzima wa simu na kusababisha kukosa mawasiliano ambayo kw adunia ya leo
tunayahitaji sana ili tuendelee,Mfano simu kuwa nzito,Kusahau msimbo wa
usalama wako,(password,Patern).ili kuyamaliza matatizo haya hapa
nakuletea trick mbalimbali za kupambana na matatizo haya
KUWASHA SIMU ILIYOZIMA
Kwa tatizo lolote ambalo simu yako ya androids haiwaki, kuna hatua nyingi za kufuata ili kutatua tatizo hili hapa nitakueleza kwa undani zaidi kukabiliana na tatizo hili.
__yawezekana simu yako imezima kutokana na betri yako kuisha chaji kabisa,Hapo chaji simu yako kisha iwashe baada ya dakika thelathini kisha ijalibu
__Kama bado haiwaki toa betri yako na jaribu betri nyingine inayofanana na betri yako,jaribu kuiwasha simu yako,ikiwa bado hili tatizo lipo
__Kama bado haiwaki na hiyo simu ilizima yenyewe bila matatizo mengine kama kuingia maji kuangushwa au kujipiga shoti,chukua waya wa usb na jaribu kuichomeka simu yako kwenye computer ijazame kama computer inaitambua hiyo simu .kamainaitambua hiyo simu itakuwa na tatizo la software inayoiongoza hiyo simu, na suluhihso lake ni kuiflashi ntakuelekeza hapo chini usijali,kama haiitambui maana yake nishati ya nguvu(power ) haifanyi kazi kwenye hiyo simu muhimu ni kumtafuta mtaalamu wa hiyo simu maana hapa utahitaji vipimo sahihi kufumbua hili tatizo waweza nicheki kwa no za simu juu hapo